- 276 viewsDuration: 3:48Shughuli za wazee wa Kaya Gandini na Kaya Mtswakara eneo la Kinango katika kaunti ya Kwale zimetatizika kwa muda kutoka na uharibifu wa vifaa vya kitamaduni wanavyotumia kufanyia maombi, matambiko na ibada maalum. Baadhi ya vifaa hivyo ni vinu na vyungu vinavyowekwa kwenye sehemu maalum katika kaya hizo huku njia za kufika kwenye Kaya zikiwa zimeharibika kutokana na mvua ya msimu uliopita. Wazee Wanasema gharama ya kurejesha vifaa hivyo iko juu na huenda maombi wanayofanya mwezi Machi yakaathirika.