Zaidi ya wafanyikazi 400 kutoka Serikali ya Kaunti ya Kajiado walioko Kajiado Kaskazini walikusanyika katika mjini Ngong kwa ibada maalum ya maombi.
Ibada hiyo ililenga kuimarisha umoja, mshikamano na kuomba mwongozo wa Mwenyezi Mungu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kuwahudumia wananchi. Akizungumza katika hafla hiyo, waziri wa ardhi, kajiado Hamilton Parseina alisisitiza umuhimu wa uadilifu kazini, akisema mtumishi wa umma anapaswa kufanya lililo sahihi hata pale ambapo hakuna anayemwangalia. Waliwahimiza wafanyakazi kufanya kazi kwa haki, uwajibikaji na busara ili kuendeleza kaunti na kuboresha huduma kwa wananchi.