- 2,762 viewsDuration: 2:56Wakenya wawili wamewasilisha kesi mahakamani kupinga mkataba uliotiwa saini hapo jana kati ya kaunti ya Nairobi na serikali ya kitaifa kuhusu usimamizi wa majukumu ya jiji hili kuu. Kulingana na wawili hao, Benard Peter na Christine Gathoni, mkataba huo umekiuka sheria na hatua hiyo ni hujuma kwa ugatuzi. Wawili hawa wanaitaka mahakama kutupilia mbali mkataba huo uliosainiwa ikulu hapo jana