Wakazi ambao nyumba zao zilibomolewa Malindi walalamika

  • | Citizen TV
    440 views

    Wakazi ambao waliathirika baada ya nyumba zao kubomolewa na baadaye kufurushwa kutoka kwa makazi hayo Malindi wanalalamikia unyanyasaji. Wakazi hao ambao wanadai kuwa walifurushwa licha ya kuwa na hati miliki za ardhi katika kijiji cha Pindukiani kaunti ndogo ya Malindi wanasema hatua hiyo ilikwenda kinyume na sheria. Zaidi ya familia 200 zimeathirika na wamelazimika kulala nje kwenye vibanda walivyojenga baada ya nyumba zao kubomolewa