Muamuzi wa kike wa Kombe la Dunia barani Afrika

  • | BBC Swahili
    2,438 views
    Ikiwa zimebaki siku chache tu kuanza kwa Kombe la Dunia nchini Qatar, kwa mara ya kwanza katika michuano hiyo kutakuwa na wasimamizi wa mechi wa kike. Kutoka Afrika atakuwa Salima Mukansanga kutoka Rwanda Mapema mwaka huu, Mnyarwanda huyo aliweka historia, ya kuwa mwanamke wa kwanza kuchezesha mechi ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanaume. Na sasa ataweka tena historia kwenye jukwaa la kimataifa. Mwandishi wa BBC alizungumza naye wakati wa mazoezi kabla ya safari yake ya Qatar. #bbcswahili #qatar2022 #worldcup #fifa #wanawake