Skip to main content
Skip to main content

Wafanyibiashara walalamikia uchafu na taka mitaani Isebania

  • | Citizen TV
    292 views
    Duration: 2:24
    Wafanyabiashara na wakazi wa Isebania wanalalamikia mirundo ya taka na uchafu karibu na maeneo ya biashara kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa. Kwa mujibu wao, taka hiyo ilitolewa kwenye mitaro wakati wa zoezi la usafi, lakini iliachwa katika maeneo ya biashara bila kuchukuliwa na kupelekwa kwenye sehemu rasmi ya kutupia taka..... Mwenyekiti wa wafanyabiashara eneo la Isebania, Samuel Kiboye, amesema serikali ya kaunti imeshindwa kutimiza wajibu wake wa kuhakikisha taka inaondolewa ipasavyo, hali inayosababisha mazingira machafu yanayoathiri biashara na afya ya wakazi. Wafanyabiashara wanasema hali hiyo imewafanya wateja kukwepa eneo hilo, huku wengine wakivuka mpaka kwenda kununua bidhaa katika nchi jirani kutokana na harufu mbaya na uchafu uliokithiri.......