- 238 viewsDuration: 1:38Zaidi ya wanafunzi 150 kutoka familia maskini katika shule ya msingi ya Kilimani kaunti ya Lamu wana sababu ya kutabasamu baada ya msamaria mwema kujitolEa kuwalipia karo ya shule.. Wanafunzi hao ambao walikuwa wamelazimika kusalia nyumbani kwa kukosa karo sasa wakiwa na matumaini. Kwa muda watoto hawa wanapoenda shuleni wamekuwa wakirudishwa nyumbani mara kwa mara wakitakiwa kuleta karo, jambo ambalo limekuwa likiathiri masomo yao pakubwa..