Skip to main content
Skip to main content

| Mwanamke bomba | Sarah November husaidia kukwamua msongamano bila malipo |

  • | Citizen TV
    3,474 views
    Duration: 5:34
    Sarah November ni mkaazi wa Baba Dogo, mtaani Kasarani, kaunti ya Nairobi. Ni mzaliwa wa Gatanga huko Muranga na hujishughulisha na kukwamua msongamano wa magari katika Barabara kuu ya Thika. Sarah ambaye hufanya kazi hiyo bila malipo yoyote anahudumu katika maeneo ya muthaiga, ngara, na pangani hapa jijini Nairobi. Licha ya shughuli hizo nyingi, Sarah pia huwafunza watu mbinu za kudhibiti moto na utunzaji wa mazingira. Kwenye Mwanamke Bomba hii leo, tunamvisha taji Sarah November