Skip to main content
Skip to main content

Citizen yaomba radhi kwa Keith Chacha kutokana na taarifa zilizomhusisha na kifo cha Elvis Munene

  • | Citizen TV
    2,380 views
    Duration: 46s
    Kwenye taarifa zetu za Nipashe zilizopeperushwa tarehe 21 Februari 2025 saa moja jioni, tuliangazia taarifa kuhusu kifo cha Elvis Munene ambaye aliripotiwa kutoweka tarehe 29 mwezi Januari, 2025. Taarifa hiyo huenda ilieleweka kumhusisha Keith Chacha na kifo hicho. Uchunguzi wetu umebaini kuwa Keith Chacha hakuhusika kwa vyovyote vile na kifo hicho. Taarifa hiyo huenda ilimwonyesha Keith Chacha kwa njia isiyostahili na hatukukusudia kumwonyesha katika hali hiyo. Tunaomba radhi kwake Keith Chacha na familia yake kutokana na hali hiyo iliyotokana na taarifa zetu.