Gavana wa Nandi aitaka serikali kusitisha uagizaji wa mahindi nje

  • | Citizen TV
    810 views

    Mwenyekiti wa magavana wa kaskazini mwa bonde la ufa Stephen Sang ameitaka serikali kusitiza uagizaji wa mahindi kutoka nchi za kigeni sasa ambapo wakulima wengi nchini wanaendelea kuvuna zao hilo. sang ameitaka serikali badala yake kununua mahindi kutoka kwa wakulima.Akizungumza mjini Kapsabet,Sang amewarai wabunge kuunda sheria itakayodhibiti kilimo na biashara ya zao la mahindi na vilevile kumwagiza waziri wa biashara na viwanda Moses Kuria kufika bungeni kuelezea mikakati ya serikali kulinda wakulima wa mahindi