- 14,984 viewsDuration: 3:24Kenya sasa imeanza kukadiria hasara ya mamilioni ya fedha kufuatia vita vya Israel na Marekani dhidi ya Iran. Wafanyibiashara wanaosafirisha nje maua, nyama na majani chai wamepata hasara ya mamilioni ya pesa katika kipindi cha siku sita ambazo vita hivyo vimekuwa vikiendelea. Shirika la ndege nchini Kenya airways, limetangaza usafiri wa kwanza wa ndege maalum leo jioni kuwarejesha nyumbani wakenya ambao wamekwama Dubai