Polisi wawakamata washukiwa watatu wa uhalifu na kunasa bunduki tatu eneo la Trans Nzoia

  • | Citizen TV
    1,038 views

    Polisi katika kaunti ya Trans Nzoia wamewakamata washukiwa watatu wa uhalifu na kunasa bunduki tatu. Hii ni kufuatia operesheni ya kuwasaka wahalifu ambao wamekuwa wakiwahangaisha wakaazi. Kamanda wa polisi katika kaunti hii Nelson Taliti anasema hii ni mojawapo ya mikakati ya kudumisha usalama Trans-Nzoia, kufuatia visa vya awali vya wizi wa mabavu madukani.