CMD yatoa ripoti inayoonyesha vyama vya kisiasa nchini vina ubaguzi

  • | Citizen TV
    279 views

    Ripoti ya kituo cha demokrasia ya vyama vingi CMD imeonyesha kwamba watu wenye mahitaji maalum hawakupewa nafasi sawa na wale wasio na mahitaji hayo katika uchaguzi mkuu ulipita. Walemavu, wanawake, vijana na wanaotoka katika jamii zilizotengwa walikabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za kifedha pamoja na kushurutishwa na vyama vya kisiasa kuwapisha wagombea waliopendelewa. Kulingana na ripoti hiyo iliyozinduliwa hapa jijini Nairobi, hatua hiyo ya ubaguzi iliwafungia nje viongozi ambao wangelifaa taifa la Kenya.