- 1,787 viewsDuration: 6:23Clive Gisairo- Mbunge, Kitutu Masaba: Kama Rais anataka kupambana na ufisadi, aanze na jumba lake, kwa sababu ufisadi uko ndani ya Ikulu kabla hata hajafika Bungeni. Kwa majuma machache tumeona mabasi yakisafirisha vijana na kila mmoja kupewa elfu kumi, pesa ambazo haziko kwenye bajeti. Kazi ya Rais si kuwapa vijana pesa, bali kuunda miundomsingi itakayowanufaisha. Tukitaka kupiga vita ufisadi, lazima tumtafute yule anayetoa hizo hela na aeleze zimetoka wapi.