Naibu rais asema awataja anaodai waliiba pesa za umma

  • | Citizen TV
    5,551 views

    Naibu rais Rigathi Gachagua sasa anasema atawataja watu anaosema walipora zaidi ya shilingi bilioni 24, miezi mitatu kabla ya mwisho wa utawala wa rais mstaafu Uhuru Kenyatta. Gachagua aliyezungumza wakati wa ibada eneo la Roysambu alidai kuwa hali ngumu ya kiuchumi inashuhudiwa sasa nchini inatokana na uporaji huo, anaodai ulifanyika na baadhi ya mawaziri na makatibu wa serikali ya Kenyatta.