- 1,643 viewsRais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi amemteua aliyekuwa makamu wa rais wa nchi hiyo Jean-Pierre Bemba, ambaye alikuwa gerezani kwa zaidi ya miaka 10 kwa uhalifu wa kivita, kuwa waziri wa ulinzi wa nchi hiyo katika mabadiliko makubwa kwenye serikali. Uteuzi wake ulikuwa sehemu ya mabadiliko makubwa ya maafisa 57 wa serikali, ambayo msemaji wa rais alisema ni ya "haraka na lazima", katika tangazo kupitia kituo cha televisheni ya taifa ya Kongo. Rais huyo pia amemteua Vital Kamerhe, mkuu wake wa zamani wa utawala, ambaye aliachiliwa kutoka gerezani mwezi Desemba 2021 baada ya kupatikana na hatia ya ubadhirifu, wakati alipokuwa waziri wa Fedha. Kamerhe Juni mwaka 2022 alifutiwa mashtaka yote baada ya kukataa rufaa dhidi ya mashtaka hayo. Mabadiliko hayo, ambayo yalikuwa makubwa zaidi kuliko ilivyotabiriwa, yamekuja kabla ya uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Desemba 20, ambapo Tshisekedi anatarajiwa kuwania muhula wa pili. #felixtshisekedi #vitalkamerhe #JeanPierreBemba #drc #mawaziri #uteuzi #congo #voa #voaswahili #dunianileo #rais - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.
Raia wa DRC aeleza faida ya uteuzi wa Kamerhe kuwa Waziri
- 30 Apr 2024 - 28 people are still missing from the killer floods in Mai Mahiu, Nakuru County, that have so far claimed the lives of 71 residents.
- 30 Apr 2024 - Former President Uhuru Kenyatta has pledged a Ksh.2 million donation to Kenya Red Cross Society to support those affected by the floods that continue to wreak havoc and claim lives across the country.
- 30 Apr 2024 - Three more bodies have been retrieved from River Tana, bringing the total number of casualties to 7.
- 30 Apr 2024 - About 30 Ukrainian men have died trying to illegally cross Ukraine's borders and avoid fighting in the war against Russia which started in 2022
- 30 Apr 2024 - Eric Nyadimo, the Institution of Surveyors of Kenya president, has pointed out the government’s failure to conduct regular mapping of the country as a key factor in the extent of havoc wreaked by ongoing rains.
- 30 Apr 2024 - James Wanjohi, a businessman identified as a city pastor has come out to deny allegations that he obtained Ksh.600 million after defrauding 4,000 Kenyans while promising them Visas to travel abroad.
- 30 Apr 2024 - Border disputes have led to the destruction of properties in towns like Keroka, but a new law could see the Senate play a crucial role in solving disputes before chaos errupts.
- 30 Apr 2024 - One of the lucky farmers selling the cattle to Ruto has been identified as Obert Chinhamo.
- 30 Apr 2024 - The government of Kenya has confirmed 71 deaths following Monday flash floods in Mai Mahiu area, Deputy President Rigathi Gachagua has said.
- 30 Apr 2024 - The government invited Kenyans to apply before the May 3, 2024 deadline.