- 379 viewsDuration: 2:05Wakazi wa mji wa Kenol, hususan vijana, wamepinga vikali mpango wa serikali wa kupanua ofisi za utawala wa Murang’a Kusini katika uwanja wa Kimorori. Kulingana nao, wamekuwa wakitumia uwanja huo kukuza vipaji vyao kupitia michezo, na sasa wanahofia kufurushwa. Vijana hao wanasema serikali inafaa kuuboresha uwanja huo ili ufikie viwango vya kisasa na kusaidia vijana kuendeleza vipaji vyao.