- 274 viewsDuration: 2:29Ni afueni kwa zaidi ya familia 10,000 katika kaunti ya vihiga baada ya serikali ya kaunti hiyo kuwasambazia maji ya mifereji kwenye maboma yao kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Akizindua baadhi ya miradi hiyo ya maji kwa wakazi wa vihiga gavana wa kaunti hiyo dkt. Wilber ottichilo amedokeza kuwa atahakikisha kwamba wakazi zaidi wanapata maji nyumbani.