- 269 viewsDuration: 3:07Ujumuishaji wa kilimo kisichotumia udongo pamoja na ufugaji wa samaki na kuku umempatia mkulima mmoja katika Kaunti ya Kiambu mavuno bora kutokana na mbinu hiyo endelevu inayotumia rasilmali chache kupata mapato ya kuridhisha. Mbinu hiyo inamwezesha kuongeza uzalishaji, kuokoa maji, mbolea na kutumia kipande kidogo tu cha ardhi. Denis Otieno alitembelea shamba la Monica Mungai na anaangazia mfumo huo wa kilimo kwenye makala ya leo ya Kilimo Biashara.