- 5,419 viewsDuration: 1:31Kinara wa DCP Rigathi Gachagua ametaka serikali kuchukua hatua za dharura na kuwaondoa wanajeshi kutoka jubaland wanaodaiwa kukita kambi kaunti ya mandera. Akizungumza katika hafla ya mazishi huko Mathioya, kaunti ya Muranga, Gachagua amesema kimya cha baadhi ya maafisa wakuu serikalini na kupuuzwa kwa madai hayo kunazua wasiwasi, akisisitiza kuwa upinzani hautasalia kimya hadi hatua zakuwahakikishia wakazi wa mandera usalama zichukuliwe.