Viongozi wa UDA wakataa kushirikiana na gavana Ole Lenku katika kaunti ya Kajiado

  • | Citizen TV
    1,647 views

    Wanachama na Viongozi wa chama cha UDA Katika kaunti ya Kajiado wametofautiana vikali na pendekezo la katibu wa chama hicho Cleophas Malala kuhusu kuzika tofauti zao za kushirikiana na Gavana wa Kaunti hiyo Joseph Ole Lenku.Wakizungumza kwenye mkutano wa wanachama huko Kajiado, wanachama hao wanalalamika kuwa Gavana Lenku amekuwa akitafuta mwafaka na Viongozi wakuu serikalini lakini anaendeleza uhasama wa kisiasa dhidi ya viongozi wa UDA Kajiado. viongozi hao wanasema kuwa hawako tayari kushirikiana na Gavana Lenku.