Mswada wa fedha watarajiwa kuwasilishwa bungeni kwa somo la pili leo

  • | Citizen TV
    2,191 views

    Mswada wa fedha wa mwaka 2023 leo unatarajiwa kuwasilishwa katika bunge la kitaifa kusomwa mara ya pili. Kamati ya Fedha katika bunge hilo inatarajiwa kuuwasilisha pamoja na marekebisho kadhaa. Mswada huu unawasilishwa huku macho yote yakielekezwa bunge kufuatia tetesi na pingamizi kali zilizojitokeza. Viongozi wa upinzani wameshikilia kuwa wataupinga mswada huo huku wale wa kenya kwanza wakisisitiza kuwa wataupitisha.