Kituo cha redio cha Kitwek FM chaadhimisha siku ya wajane ulimwenguni kwa kutoa Sodo na miche

  • | KBC Video
    12 views

    Kituo cha redio cha Kitwek FM kinachomilikiwa na shirika la utangazaji la Kenya KBC kiliadhimisha siku ya wajane ulimwenguni na wanawake kutoka Chemegong eneo la Soin/Sigowet, kaunti ya Kericho. Wafanyakazi wa kituo hicho walitoa Sodo, miche na vifaa vingine kwa ushirikiano na mchakato wa “Mama Doing Good”, unaoongozwa na mama wa taifa Rachael Ruto. Washirika wengine waliokuwepo ni pamoja na shirika la huduma kwa misitu nchini na chama cha ushirika cha Imarisha.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channell: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1news Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #widowsday #dirayamagwiji