Waumini wa dini ya kiislamu washeherekea siku ya Eid ul adha katika maeneo tofauti nchini

  • | Citizen TV
    258 views

    Kwa siku ya pili waumini wa dini ya kiislamu wanasheherekea siku ya Eid ul adha katika maeneo tofauti nchini. katika kaunti ya mombasa, Gavana ABDULSWAMAD SHARRIF NASSIR amewataka waislamu kudumisha umoja na kuwakumbuka wasiojiweza. Akiongea katika uwanja wa Ronald ngala ambapo alijiunga na mamia ya waislamu kwa sherehe hizo Sharrif Nassir ametaka serikali kutatua suala la gharama ya Maisha. Aidha viongozi wa kidini kutoka mombasa wametaka tume ya huduma za mahakama JSC kuharakisha uteuzi wa kadhi mkuu na kushikilia kwamba zoezi hilo ni sharti liwe na uwazi.