Je, Ruto alikiuka katiba alipowaidhinisha washauri wake kuhudhuria mikutano ya baraza la mawaziri?

  • | Citizen TV
    662 views

    Je, Rais William Ruto alikiuka katiba alipowaidhinisha washauri watatu pamoja na katibu mkuu wa chama cha UDA Cleophas Malala kuhudhuria mikutano ya baraza la mawaziri? Ndio suala kuu miongoni mwa wanasheria ikizingatiwa kwamba hatua ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kumhusisha aliyekuwa mkurugenzi wa Huduma za jiji la Nairobi Mohamed Badi iliharamishwa na mahakama kwa msingi kuwa Katiba haimpi Rais mamlaka yoyote ya kumhusisha mgeni katika shughuli za baraza la Mawaziri.