Murang'a Seal yakung'uta Shabana FC

  • | Citizen TV
    1,229 views

    Timu ya Murang'a Seal imesitisha kwa muda sherehe za Shabana FC na ushindi wa mabao 2-1 mjini Murang'a. Shabana ilihitaji pointi moja ili kunyakua ubingwa wa ligi kuu ya daraja la pili. Murang'a Seal walianza kwa kishindo na bao lake Fabian Adikiny katika dakika ya saba. Maji yalizindi unga kwa Shabana pale Murang’a walipoongeza bao la pili katika dakika ya 36, kombora lake Ally Yusuf likimchanganya kipa wa Shabana. Katika kipindi cha pili, Shabana ilipata bao la kufutia machozi baada ya Geoffrey Onyango kupiga kichwa safi katika dakika ya 76. Shabana inaongoza ligi pointi mbili mbele ya Murang’a ikisalia raundi moja pekee ligi kukamilika.