Shughuli za uokoaji zaendelea kuwatafuta waliozama katika Ziwa Victoria

  • | Citizen TV
    431 views

    Shughuli za uokoaji zinaendelea katika ziwa Victoria baada ya boti iliyokuwa imewabeba watu 11 kuzama hapo jana nchini Uganda. Kwa mujibu wa polisi nchini humo, watu watano waliokuwa wakisafiri kutoka visiwa vya Kiseba kuelekea mukono hawajulikani waliko. Watu wengine sita waliokolewa kwenye tukio hilo, japo haikubainika mara moja wakati ajali hiyo ilipotokea. Ajali hii ya punde ikijiri siku moja baada ya boti nyingine iliyokuwa imebeba vyakula kutoka visiwa vya kasi kuzama, na kumuua mtu mmoja huku mwingine akiokolewa na wavuvi.