Wanafunzi wengi waathirika macho Kaunti ya Uasin Gishu

  • | Citizen TV
    175 views

    Muda mwingi ambao wanafunzi wanatumia katika shughuli za masomo, na kukaa muda mrefu darasani bila kutoka nje, au kutazama ubao mweupe kwa muda mrefu ni baadhi ya sababu ambazo zimetajwa kuchagia kuumiza afya ya macho yao. katika kaunti ya Uasin Gishu, Wanafunzi takribani elfu tatu ambao walifanyiwa vipimo vya macho walipatikana kuwa na matatizo. Hali hiyo inaarifiwa kuathiri masomo yao haswa iwapo hawatafuti matibabu ya kutatua shida hiyo mapema