Kundi la kina mama wa kiislamu lasafisha mji wa Kajiado kwa kuzoa taka ambazo zimetapakaa

  • | Citizen TV
    516 views

    Kundi moja la kina mama wa kiisilamu kutoka mji wa Kajiado Limejitwika jukumu la kuanza kusafisha mji huo kwa kuzoa taka ambazo zimetapakaa katika sehemu tofauti na kuziba mitaro ya kupitisha maji kwenye mji huo. Kina mama hao wanasema wamechukua hatua hiyo ili kuchangia kwenye juhudi za kusafisha mazingira hasa katika mji wa Kajiado ambao kwa mara nyingi kero ya taka kutapaa ovyo imekuwa changamoto ya muda mrefu.