Katika hatua inayodhamiriwa kupiga jeki juhudi za kutokomeza ugonjwa wa kupooza pamoja na michipuko ya maradhi mengine humu nchini, wizara ya afya imezindua maabara pana ya kushughulikia ugonjwa huo katika taasisi ya utafiti wa matibabu -KEMRI jijini Nairobi. Akiongea wakati wa uzinduzi huo leo, waziri wa afya Aden Duale, alithibitisha kwamba kituo hicho kitasaidia kuimarisha mifumo ya kubaini mitindo ya chembechembe za msimbojeni na kupiga jeki sekta ya afya katika kanda hii.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive