Jamii kwenye mpaka wa Nandi na Kisumu wahusishwa kwenye sanaa ya amani

  • | Citizen TV
    232 views

    Ukosefu wa amani mara kwa mara kwenye mpaka wa Nandi na Kisumu umekuwa ukisababishwa na mzozo wa mpaka ,wizi wa mifugo na hata uchochezi wa kisiasa.Eneo hilo hata hivyo limepata taswira tofauti kutokana na juhudi za kuleta pamoja jamii zinazoishi kwenye mpaka kupitia kwa mIchezo densi na uigizaji.Wanaharakati wa amani wamekuwa wakifanya hamasa ili kuwasaidia wakazi kutangamana na kuishi kwa amani na kuweka tofauti zao katika kaburi la sahau.