Shirika la IGAD kwa ushirikiano na serikali za Kenya na Ethiopia kuimarisha mahusiano mpakani

  • | KBC Video
    28 views

    Jamii za mpakani mwa Kenya na Ethiopia sasa zitafurahia ushirikiano wa kikanda na kuimarishwa kwa usafirishaji wa bidhaa na huduma. Haya yanajiri baada ya mataifa wanachama wa shirika la IGAD kwa ushirikiano na serikali za Kenya na Ethiopia kuzindua afisi ya kuwezesha maendeleo ya mipaka ya IGAD katika mpaka wa Moyale ili kuimarisha mbinu iliyoratibiwa ya kufanikisha ushirikishwaji wa shirika hilo wakati wa changamoto zozote katika eneo hilo. Zikipongeza hatua hiyo, jamii hizo kutoka kwa mataifa hayo mawili jirani, zilihimiza uingiliaji kati zaidi ili kurahisisha biashara na kutokomeza migogoro baina ya jamii za mipakani mara moja.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News