Visa vya watoto kutelekezwa katika kaunti ya mpakani ya Busia vinazidi kuongezeka

  • | Citizen TV
    468 views

    Visa vya watoto kutelekezwa katika kaunti ya mpakani ya Busia vinazidi kuongezeka huku watoto hao walio chini ya umri wa miaka 18 wakinyimwa haki zao za kimsingi. Takwimu kutoka idara ya watoto Busia zinaashiria kuwa idadi ya visa hivyo imefikia asilimia 58 huku wengi wa wazazi wanaopuuza mahitaji ya kimsingi ya wanao, wakiwa ni wa na umri wa kati ya miaka 15 hadi 25.