Babu Owino ataka elimu iwe bure kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu

  • | K24 Video
    22 views

    Hoja inayolenga kuongeza ufadhili wa masomo kwa kila mwanafunzi kutoka shilingi elfu moja mia nne hadi elfu saba ikiwa na kusudi ya kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula shuleni imewasilishwa bungeni. Kulingana na mwenye hoja ambaye ni mbunge wa Gatanga Edward Muriu, hoja hiyo pia inapendekeza fedha zinazotengewa maendeleo ya maeneo bunge zitumike vile vile kufadhili wanafunzi wa shule za msingi.