Muislamu kutengeza majeneza ya wakristo? Nilitengwa na familia!

  • | BBC Swahili
    961 views
    Tatizo la ajira nchini Tanzania, limewasukuma baadhi ya vijana kujiingiza katika biashara ambazo zinaonekana kukinzana na imani za kidini, mila pamoja na desturi zao. Atwai Mwinyi Mkaga ni kijana aliyejiingiza katika utoaji wa huduma za kutengeza majeneza na hivyo kutokana na imani yake ya dini ya kiislamu, alijikuta akiwa na wakati mgumu ikiwemo kutengwa na familia yake ambayo awali haikufurahishwa na biashara ya kutengeza majeneza kwa waktristo. Atwai maarufu kwa jina la Mwinyi katika hospitali ya Mt. Meru jijini Arusha, anamsimulia mwandishi wa BBC Aboubakar Famau jinsi alivyopambana kubadilisha dhana hiyo katika jamii yake.