Chitembwe ahusishwa na madai ya ufisadi

  • | K24 Video
    109 views

    Macho yote sasa yameelekezwa kwa rais William Ruto kumwondoa afisini rasmi jaji aliyesimamishwa kazi baada ya mahakama ya juu kutupilia mbali rufaa yake ya kupinga mapendekezo ya jopo lililoteuliwa kuchunguza utendakazi wake na kupendekeza kutimuliwa kwake kutoka kwa idara ya mahakama. Jopo hilo lilimpata jaji Chitembwe na makosa manne yaliyokiuka maadili yaliyowekwa kwa majaji wa mahakama ya juu zaidi. Kesi hiyo inatokana na kesi ya ufisadi inamhusisha gavana wa zamani wa Nairobi Mike Sonko aliyetoa kanda za video zilimhusisha Chitembwe.