Skip to main content
Skip to main content

Shabiki akamatwa kwa kukejeli bendera ya Kenya uwanjani

  • | Citizen TV
    18,084 views
    Duration: 1:49
    Idara ya upelelezi imethibitisha kukamatwa kwa Ibrahim Haidar yusuf, mmoja wa vijana walionaswa kwenye picha za simu wakiikosea heshima bendera ya Kenya wikendi iliyopita, wakati wa mechi kati ya Mogadishu City na Police FC. Ibrahim mwenye umri wa miaka 17 amekamatwa saa chache baada ya Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja kumuagiza Mkurugenzi wa DCI Mohammed Amin kuwasaka na kuwakamata wote walionaswa wakiikosea heshima bendera ya taifa