Makala ya Thelathini mbili ya mashindano ya kimataifa ya ngamia yamezinduliwa rasmi kaunti ya samburu na waziri wa utalii rebecca miano na kuwavutia washirika wa kimataifa pamoja na wenyeji. Ni hafla iliyosheheni mbwembwe za aina yake, ikitoa nafasi kwa washirika wa humu nchini kutoana kijasho na washirika wa kigeni na kipenga kilipopulizwa ikawa hali ya mwenye nguvu mpishe. Makala hayo ya thelathini na mbili yatafiki kikomo hapo kesho,miamba na mababe wa mashindano hayo watakaposhuka ugani kutafuta ubingwa.