Wawakilishi wadi wamkashifu Gavana Barchok Asutwa kwa kutoendeleza kaunti

  • | Citizen TV
    503 views

    Baadhi ya wawakilishi wadi wa Bunge la Kaunti ya Bomet wamemkashifu Gavana Hillary Barchok kwa kukosa kutekeleza miradi ya maendeleo licha ya kuwa na bilioni 8.5 katika mwaka wa kifedha wa 2023/2024. Wawakilishi wadi hao walidai Gavana huyo alikuwa akiwatisha kisiasa kwa kuibua masuala ya maendeleo na usimamizi wa rasilimali. Viongozi hao walisema sekta Za afya, maji na barabara zimeathirika zaidi na utumizi mbaya wa rasilimali.