Mfalme Charles III agundulika na aina fulani ya saratani
Mfalme Charles III amegundulika kuwa ana aina fulani ya saratani na ameanza matibabu, Kasri ya Buckingham imesema Jumatatu.
Kasri hiyo inasema saratani hiyo haihusiani na matibabu ya karibuni ya tezi ambayo haikuwa saratani. Haikusema ni aina gani ya saratani mfalme huyo mwenye umri wa miaka 75 anayo.
Kasri ilisema “kulikuwa na hali ya wasiwasi iliyoelezwa” wakati wa matibabu ya Charles kwa kukua kwa tezi dume mwezi uliopita. “Uchunguzi wa matibabu umegundua aina ya saratani,” ilisema.
Ilisema Charles “ameendelea kuwa mwenye fikra chanya kuhusu matibabu yake na anatarajia kurudi kutekeleza majukumu yake kikamilifu haraka iwezekanavyo.
Kasri iliongeza kuwa mfalme “amechagua kuweka taarifa za ugonjwa wake wazi kuepusha watu kueneza uvumi na kwa matumaini inaweza kuusaidia umma kufahamu hali ya wote walioko ulimwenguni ambao wameathiriwa na saratani.
Charles alitawazwa kuwa mfalme Septemba 2022 wakati mama yake Malkia Elizabeth II alipofariki akiwa na umri wa miaka 96. -AP
#saratani #maradhi #mfalmecharlesIII #uingereza #buckinghampalace #voa #voaswahili
13 Aug 2025
- The clarification follows an uproar from Kenyans.
13 Aug 2025
- The United States as intensified crackdown on individuals seeking student visas.
13 Aug 2025
- The president had previously hosted thousands of youths at State House.
13 Aug 2025
- President William Ruto on Wednesday assented to the County Allocation of Revenue Bill, 2025, and the County Public Finance Laws (Amendment) Bill, 2023.
13 Aug 2025
- The ruling follows a petition filed by four individuals, among them Nakuru-based surgeon Dr. Benjamin Gikenyi, challenging the legality of the committee appointed to audit pending NHIF claims.
13 Aug 2025
- The clarification follows an uproar from Kenyans.
13 Aug 2025
- The United States as intensified crackdown on individuals seeking student visas.
13 Aug 2025
- The president had previously hosted thousands of youths at State House.
13 Aug 2025
- China expects to import 2,000 tonnes of macadamia by the end of the year.
13 Aug 2025
- "Tusiharibu game tumestruggle sana kuijenga.”
13 Aug 2025
- The PROMISES!
13 Aug 2025
- Senior officials from the British Army Training Unit Kenya (BATUK) failed to appear in Parliament on Tuesday to answer questions about the atrocities their soldiers have committed in the country.
13 Aug 2025
- African officials and experts have warned that the unpredictability of U.S. trade policy fuels uncertainty for the continent's development.