Kijiji cha Taptengelei kiilisifiwa na Rais Ruto kuwa na kazi za tarakilishi

  • | Citizen TV
    1,932 views

    Katika siku chache zilizopita,kijiji cha Taptengelei katika eneo bunge la Tinderet Kaunti ya Nandi kimepata umaarufu hasa kwenye mitandao ya kijamii baada ya matamshi ya Rais William kuwa vijana kutoka kijiji hicho walikuwa wakibonyeza tarakilishi tu na kupokea dola kwa wingi. Jambo hili hata hivyo limezua hisia mseto miongoni mwa wakazi wa kijiji hicho. Wengi wao wakisema kuwa licha ya kijiji chao kujulikana, bado wanapitia changamoto za kujikimu kimaisha kinyume na dhana iliyoko kwenye mitandao.