- 673 viewsNdugu na jamii ya mwanariadha aliyevunja rekodi ya dunia Kelvin Kiptum huko katika Kaunti ya Elgeyo Marakwet walikusanyika nyumbani kwa nyota wa riadha Jumatatu kuifariji familia yake baada ya kusikia habari za kifo chake kilichotokana na ajali ya gari. Baba yake alilia na kughubikwa na hisia wakati alipokuwa ameketi pamoja na waliokuja kuomboleza. Samson Cheruyot, mkulima, alisema Kiptum alitarajia kubadilisha hali ya familia yake kwa umaarufu alioupata ghafla, na walikuwa wamezungumzia kujenga nyumba na kuipatia familia yake gari. “Hivi sasa sijui niseme nini; hivi sasa kila mmoja ananiangalia mimi, hatujui tufanye nini,” Cheruyot alisema. Mkewe, Asenath Cheruto Rotich, alisema kuwa Kiptum alikuwa ni baba mwenye mapenzi kwa watoto wake. Rotich alisema alikuwa na wasiwasi kuhusu maisha ya watoto wao wawili na kuiomba serikali kumsaidia. “Ninaiomba serikali inisaidie ili niweze kuwasaidia watoto hawa kama baba yao alivyokuwa anawasaidia. Alikuwa anawapenda watoto wake, sijui hata kile ambacho nitawaambia,” alisema. Ilikuwa wiki chache zilizopita Kiptum aliapa kuvunja rekodi yake mwenyewe ya dunia kuwa mwanariadha wa kwanza kumaliza mbio za marathon chini ya saa mbili katika mashindano yajayo ya Rotterdam mwezi Aprili, na pia kujitokeza kwa mara ya kwanza katika mashindano ya Olimpiki huko Paris kipindi cha joto. Ndoto hiyo imekufa Jumapili wakati baba huyo wa watoto wawili mwenye umri wa miaka 24 alipofariki akiwa pamoja na kocha wake katika ajali ya gari huko Rift Valley. Polisi ilisema mwanariadha huyo alipoteza udhibiti wa gari alilokuwa analiendesha na kuacha njia akitumbukia katika shimo, akiwa amesafiri umbali wa takriban kilomita 0.06 kabla ya kugonga mti mkubwa. #Kenya #Kelvin #Kiptum #death #family #mourn #VOAAfrica
Baba, Mke na Wanafamilia wamlilia Hayati Kiptum
- 6 Jul 2025 - Traders affected by the recent demonstrations held in honour of victims of last year’s anti-Finance Bill protests are now struggling to rebuild their lives and livelihoods.
- 6 Jul 2025 - Deputy President Kithure Kindiki and other leaders backing the broad-based government have intensified attacks on the opposition, calling for unity to heal the nation.
- 6 Jul 2025 - The High Commission of Rwanda in Kenya has marked 31 years of liberation — a commemoration of the country’s remarkable transformation, from a painful past under an oppressive regime to a future defined by unity, progress, and resilience.
- 5 Jul 2025 - Opposition leaders have come out guns blazing to condemn President William Ruto's stance on constructing a church within the State House precincts, using what the president describes as his own money.
- 5 Jul 2025 - A family in Eldoret, Uasin Gishu County, is mourning the loss of their son, Timothy Bwibo, who succumbed to gunshot injuries on Friday night.
- 5 Jul 2025 - Former Meru Governor Kawira Mwangaza has been named the new party leader of Umoja na Maendeleo Party, taking over from Charles Wambora Mugambi.
- 5 Jul 2025 - National Assembly Speaker Moses Wetang’ula has faulted the trend of tribal and divisive politics, cautioning that such narratives risk plunging the country into dangerous polarization.
- 5 Jul 2025 - President William Ruto has replaced former Kesses Member of Parliament Dr. Swarup Mishra as the chair of the Kenya BioVax Institute, three months after suspending him.
- 5 Jul 2025 - James McMurdock denies any wrongdoing over claims relating to pandemic-era loans taken out by his companies.
- 5 Jul 2025 - Kenya’s road to the 2025 World Athletics Championships in Tokyo enters a decisive phase on Saturday, July 5, 2025, as the Prefontaine Classic in Eugene, Oregon, doubles as the national trials for the women’s 5,000m and men’s 10,000m races. While reigning…