Mimi, Kikeke tulikuwa watangazaji wa kwanza wa Kombe la Dunia kwa Kiswahili

  • | BBC Swahili
    3,370 views
    Miaka 65 ya BBC Swahili. Hiki ndicho anachojivunia Charles Hillary aliyewahi kufanya kazi na Idhaa ya Kiswahili ya BBC akiwa ni mmoja ya watangazaji mashuhuri sana hasa katika matangazo ya moja kwa moja ya mpira wa miguu yaliyokuwa yakitangazwa na Idhaa ya Kiswahili ya BBC. Kwa sasa ni Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu visiwani Zanzibar Lakini anakumbuka nini hasa siku yake ya kwanza alipojiunga na BBC Swahili? Mwandishi wa BBC alimtembelea Ikulu ya Zanzibar na nilizungumza nae. #bbcswahili65 #bbcswahili #tanzania