Gavana wa Kakamega aunga mkono azma ya Raila ya kuwania wadhifa wa mwenyekiti wa AUC

  • | Citizen TV
    1,818 views

    Gavana wa Kakamega Fernandes Barasa amuunga mkono azma ya kinara wa Azimio Raila Odinga ya kuwania wadhifa wa mwenyekiti wa tume ya muungano wa Afrika. Aidha Barasa anapinga dhana kuwa jukumu hilo litapunguza ushawishi wa kisiasa wa Odinga kitaifa. Ikiwa atachaguliwa na wanachama 53 wa tume ya muungano wa Afrika, odinga atakuwa madarakani hadi 2029, mwaka mmoja baada ya uchaguzi mkuu ujao wa Kenya.