Idadi ya vifo kutokana na ajali zilizotokea katika eneo la Kikopei na eneo la Zambezi katika kipindi cha saa 24, imefikia watu 19. Takwimu hizi zimeibua wasiwasi kuhusu uhamasishaji wa usalama barabarani, hususan baada ya kubainika kuwa ajali ya Kikopei iliua watu 16 kutoka familia moja. Mwenyekiti wa chama cha usalama barabarani humunchini, David Kiarie, sasa anatoa wito wa kusitishwa mara moja kwa leseni za madereva zilizotolewa katika kipindi cha miaka sita iliyopita, pamoja na mafunzo mapya kwa madereva. Anadai kuwa leseni nyingi zilipatikana kwa njia zisizo halali.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive