Ukosefu wa ajira kwa vijana unasalia kuwa mojawapo ya changamoto kubwa nchini Kenya, huku Wakenya waliohitimu wakiwa miongoni mwa vijana zaidi ya milioni 12 wa Afrika wanaojiunga na soko la ajira. Haya ni kwa mujibu wa Benki ya Dunia, ambayo inasema zaidi kuwa karibu asilimia 70 ya vijana kwa sasa wamekwama katika ajira za kiwango cha chini, huku ajira rasmi zipatazo milioni 3 pekee zikitolewa kila mwaka. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chuo cha Benki ya Dunia cha African Skills for Job Policy Academy jijini Nairobi siku ya Jumanne, Katibu wa vyuo vya kutoa mafunzo ya kiufundi Dkt. Esther Muoria alisema serikali inabadilisha elimu na mafunzo kuwa ya vitendo, yanayoendeshwa kulingana na mahitaji, na kuakisi soko la ajira katika jitihada za kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira linaloongezeka miongoni mwa vijana kila kuchao.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive