Maafisa kliniki nchini waendeleza mgomo wao leo hii

  • | Citizen TV
    168 views

    Maafisa kliniki kote nchini wameanza mgomo wao, huku huduma za matibabu zikiendelea kutatizwa na mgomo wa madaktari ulioendelea kwa siku ya 20 hii leo. Mgomo wa maafisa hawa ukianza baada ya ilani ya siku saba kukamilika. Mgomo huu sasa umeathiri huduma muhimu za matibabu, ambazo sasa zimewalazimu wagonjwa kutafuta huduma kwenye hospitali za kibinafsi.