- 14,566 viewsDuration: 2:06Mabasi mapya ya Mwendokasi nchini Tanzania yameanza kubeba Abiria wa maeneo ya Mbezi - Kimara ili kuondoa kero ya usafiri iliyokuwepo katika barabara hiyo. Hii inakuja kufuatia picha za video zilizosambaa mitandaoni hapo awali zikionyesha baadhi ya vioo vya mabasi na vituo vikiwa vimevunjwa baada ya kushambuliwa kwa mawe usiku wa kuamkia leo Jijini Dar es Salaam. Pia siku za hivi karibuni njia hiyo ya usafiri inayotegemewa na maelfu ya wakaazi wa jiji hilo nchini Tanzania imekumbwa na malalamiko ya wananchi kutokana na uhaba wa mabasi ikilinganishwa na idadi ya abiria. - - 🎥@eagansalla_gifted_sounds #bbcswahili #tanzania #Usafiri #daressalaam