Raila atoa onyo kwa serikali dhidi ya kuendelea na ubomoaji na kutoa ilani za kuhamisha wanainchi

  • | K24 Video
    193 views

    Kinara wa muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga, ametoa onyo kwa serikali dhidi ya kuendelea na ubomoaji na kutoa ilani za kuhamisha wananchi bila kutoa maelekezo ya wazi ya wapi watu wanapaswa kuenda. Aidha, Odinga ameiomba serikali kutangaza mafuriko kama janga la kitaifa ili kufungua milango kwa wafadhili kutoa misaada.