Tume ya uwiano ya NCIC yaanzisha misafara ya amani, Siaya

  • | Citizen TV
    228 views

    Tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa NCIC imetaja maeneo ya Nyadorera, Siaya mjini, Sidindi na Usenge kuwa baadhi ya maeneo ambayo huenda yakawa kwenye hatari ya machafuko msimu huu wa kampeni za uchaguzi mkuu. Akihutubia waandishi wa habari mjini Siaya wakati wa kuanzisha rasmi msafara wa kuhubiri amani kaunti ya Siaya, Mkurugenzi wa utafiti katika tume ya NCIC, Millicent Okach, ameeleza kuwa lengo la msafara huo ni kuhubiri amani kuhakikisha uchaguzi salama mwezi ujao. NCIC ikipangiwa kupiga kambi kaunti ya Siaya kwa juma moja kuanzia hii leo.